Kumuwakilisha mwingine amhijie baba


Swali: Naweza kumpatia mtu mwingine pesa amhijie baba yangu aliyefariki?

Jibu: Ndio, haina neno kufanya hivo. Hata hivyo lengo la yule mwenye kuhiji isiwe pesa. Ikiwa lengo lake ni pesa hajj yake haisihi. Ama ikiwa anatumia pesa ili zimsaidie wakati wa hajj, amnufaishe yule maiti na alipwe kwa kusimama zile sehemu za ´ibaadah na kuswali kwenye msikiti Mtakatifu wa Makkah, ni sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-09.mp3
  • Imechapishwa: 25/05/2018