Kumuuliza muislamu juu ya uhalali wa chakula chake

Swali: Je, inasuniwa kwa muislamu kumuuliza muislamu mwenzake juu ya chakula alichomletea?

Jibu: Msingi juu ya chakula cha muislamu ni kwamba ni halali. Lakini akitia shaka juu ya chumo lake au akamtuhumu kutoitakasa dini yake na hayo yakatambulika na kuhifadhiwa kutoka kwake, basi katika hali hiyo muulize na hakuna kikwazo. Vinginevyo msingi ni kwamba chakula cha muislamu ni halali.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Kariym bin ´Abdillaah al-Khudhwayr
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://saif.af.org.sa/sites/default/files/fatwa4.mp3
  • Imechapishwa: 16/09/2022