Kumuuliza mtu sababu ya kumtaliki mke wake


Swali: Imekatazwa kumuuliza mtu kwa nini amemtaliki mke wake kama jinsi imevyokatazwa kumuuliza kwa nini amempiga?

Jibu: Kuna faida gani ya kumuuliza kwa nini amempiga na kumtaliki? Faida iko wapi? Ikiwa muulizaji ni Muftiy anataka kutazama kama anaweza kutengeneza hali, hakuna neno. Ama mtu wa kawaida kwa nini ajiingize!! Huku ni kujiingiza kwa mambo yasiyokuhusu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (37) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-12-29.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014