Kumuozesha binti kwa nguvu na asiyemtaka


Swali: Ni ipi hukumu ya kumuozesha binti kwa nguvu na kinyume bila ya kuchukua maoni yake?

Jibu: Ni lazima kuchukua maoni yake. Haozeshwi kwa nguvu binti isipokuwa kwa kupata idhini yake na ridhaa yake. Bikira anaombwa idhini na ambaye kishaolewa ndio anaamrishwa na wala binti asiozeshwe kwa nguvu na yule asiyemtaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/5431
  • Imechapishwa: 20/09/2020