Kumuombea Du´aa Mama Nyumbani Kwa Kutokujua Kaburi Lake Lilipo


Swali: Ikiwa nataka kutembelea kaburi la mama yangu au baba yangu na sijui mahala maalum ambapo kaburi lipo, inatosheleza kwenda makaburini na kumuombea?

Jibu: Unaweza kumuombea hata kama hukwenda makaburini. Ikiwa hukujua kaburi lake ili uliendee na kusimama mbele yake, muombee ilihali uko nyumbani kwako au mahala popote na hakuna haja ya kwenda makaburini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (11) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1430-11-6.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014