Kumuombea du´aa aliyetoa swadaqah kwa mitindo ya ki-Bid´ah

Swali: Vipi kuhusu watu wanaokusanyika kwenye swadaqah inayotakiwa kugawanywa kwao na wanaweka mikono yao juu yake na mmoja wao anamuombea du´aa yule aliyetoa swadaqah na wengine wanaitikia “Aamiyn” kwa sauti ya juu?

Jibu: Mtindo huu haufai. Kwa sababu ni Bid´ah. Ama kumuombea du´aa yule mtoaji swadaqah bila ya kuweka mkono juu ya ile mali iliotolewa swadaqah na bila kukusanyika pamoja na kunyanyua sauti kwa mtindo uliotajwa ni jambo linalokubalika Kishari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kukufanyieni wema basi mlipeni. Msipopata cha kumlipa nacho muombeeni du´aa hadi muone kuwa mmemlipa.”

Ameipokea Abu Daawuud, an-Nasaa´iy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (01/441) https://binbaz.org.sa/fatwas/38/%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%AC%D8%A7%D8%A8%D8%A9-%D8%B9%D9%86-%D8%B3%D9%88%D8%A7%D9%84-%D8%AD%D9%88%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%AF%D8%B9%D8%A7%D8%A1-%D8%B9%D9%86%D8%AF-%D8%AA%D9%81%D8%B1%D9%8A%D9%82-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D8%AF%D9%82%D8%A9
  • Imechapishwa: 29/11/2019