Swali: Tumesikia kwamba haijuzu kusema:

سامحنا يا رسول الله

“Ee Mtume wa Allaah! Tusamehe.”

Kwa sababu msamaha anaombwa Allaah pekee. Ni yepi maoni yako?

Jibu: Ndio, haijuzu. Hii ni shirki kusema:

يا رسول الله سامحني، يا رسول الله اغفر لي

“Ee Mtume wa Allaah! Nisamehe. Ee Mtume wa Allaah! Nighufurie.”

Ni shirki. Hii ni haki ya Allaah (´Azza wa Jall). Akisema:

يا رسول الله اغفر لي، يا رسول الله اشفع لي، يا رسول الله سامحني

“Ee Mtume wa Allaah! Nighufurie. Ee Mtume wa Allaah! Nitakie uombezi. Ee Mtume wa Allaah! Nisamehe.”

Kusema hivi haijuzu. Msamaha unaombwa kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si yeye ambaye analipa thawabu na kuadhibu. Ambaye analipa thawabu na kusamehe ni Allaah. Ni lazima watu kutahadhari jambo hilo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/33/%D8%B7%D9%84%D8%A8-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B3%D8%A7%D9%85%D8%AD%D8%A9-%D9%85%D9%86-%D8%B1%D8%B3%D9%88%D9%84-%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87
  • Imechapishwa: 01/12/2019