Kumuomba Mtume (صلى الله عليه وسلم) ni shirki

Swali: Ni shirki mtu akimuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hayuko mbele ya kaburi lake? Je, hukumu inatofautiana mtu akimuomba ilihali yuko mbele ya kaburi lake?

Jibu: Hapana, hukumu haitofautiani. Kumuomba asiyekuwa Allaah, popote pale, ni shirki. Haijalishi kitu mtu akiwa makaburini au mahala kwengine. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَنَّ الْمَسَاجِدَ لِلَّـهِ فَلَا تَدْعُوا مَعَ اللَّـهِ أَحَدًا

“Kwamba mahala kote pa kuswalia ni kwa ajili ya Allaah pekee, hivyo basi msiombe yeyote pamoja na Allaah.” (72:18)

فَادْعُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ

“Basi mwombeni Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini.” (40:14)

Ni lazima kumtakasia ´ibaadah katika du´aa pahali kokote. Hili halihusiani na kwenye makaburi peke yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2105
  • Imechapishwa: 30/06/2020