Swali: Ni ipi hukumu ya kumuomba msamaha maiti kwa kusema “Baba yangu nisamehe kwa niliyoyafanya” ilihali ni maiti?

Jibu: Hapana. Haijuzu. Maiti haombwi msamaha wala haiombwi kitu chochote. Baada ya kufa kwake haombwi msamaha na wala hawezi kukusamehe. Ni lazima kwako kumuombea msamaha, kumtolea Swadaqah na kufanya Tawbah kwa Allaah kwa upungufu uliofanya katika haki zake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/montqa–14340103.mp3
  • Imechapishwa: 09/08/2020