Kumuomba idhini mke wa kwanza ya kuongeza mke mwingine


Swali la kwanza: Je, ni wajibu kumtambulisha kwanza mke wa kwanza wakati mume anataka kuongeza mke mwingine?

Jibu: Hapana sio wajibu. Isipokuwa ikiwa alimshurutishia hilo. Ikiwa alimuwekea sharti ya kwamba asioe mwanamke mwingine, ni wajibu kwake kutimiza sharti hii mpake ampe idhini.

Swali la pili: Na je, ni lazima akubaliane kwanza na yule mke wa kwanza?

Jibu: Mke wa kwanza sio walii wake ili kukubaliana nae kwanza.

Muuliizaji: Sisi huku kwetu, kwa mfano Morocco unapotaka kuongeza mke, unatakiwa kukubaliana kwanza na yule mke wa kwanza.

Muhammad al-Madkhaliy Hili ni batili kwa kuwa (mke huyo wa kwanza) sio walii wake mume huyu. Yeye (mume) ndiye walii na msimamizi wake. Yeye (mume) ndiye atoae idhini anapotaka kusafiri, kutoka, kwenda katika nyumba fulani. Ama yeye (mke) kumpa idhini, haya ni makosa. Hili ni kinyume na Kauli ya Allaah (Jalla wa ´Alaa):

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ

“Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya (matumizi) wanayotoa katika mali zao.” (04:34)

Uamuzi ni wa mwanaume kwa kuwa yeye ndiye mwenye kutoa idhini na si yeye (mke). Yeye ni mke wake na wewe ni mume wake.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=NCQ5DCO4zHM
  • Imechapishwa: 21/03/2018