Kumuomba Allaah kwa haki ya waombaji

Swali: Ni ipi hukumu ya du´aa hii wakati wa kwenda msikitini:

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kwa haki ya wenye kukuomba na kwa haki ya kutembea kwangu huku kwa ajili Yako?”

Jibu: Haya yamepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakini hata hivyo juu yake kuna maneno. Haikusihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini lau tutachukulia kuwa imesihi maana yake ni kuomba kwa haki ya waombaji, lakini hata hivyo sio waombaji kwa dhati zao. Haki ya waombaji maana yake ni kujibiwa. Allaah yukaribu Mwenye kujibu. Miongoni mwa majina Yake ni Mwenye kujibia. Haki ya waombaji kwa Allaah ni Yeye kuwajibu. Wewe unamuomba Allaah kwa kitu Alichojiwajibishia Mwenyewe (Subhaanahu wa Ta´ala). Hufai kuomba kwa [haki ya] waombaji kwa dhati zao. Unachotakiwa ni kuomba kwa haki zao mbele ya Allaah ambayo ni kujibiwa. Hapa ni pale ambapo tutachukulia kuwa Hadiyth imesihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2120
  • Imechapishwa: 09/07/2020