Kumuomba Allaah Awaongoze Watu Wote


Swali: Inazingatiwa kuwa ni kupetuka mipaka katika du´aa kumuomba Allaah kwa kitu kinachoenda kinyume na utashi wa kilimwengu kama kumuomba Allaah awaongoze watu wote na awakunjulie riziki watu wote?

Jibu: Ndio, ni kupetuka mpaka. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anampotosha amtakaye na anamwongoza amtakaye. Hawaongoi watu wote na wala hawapotoi watu wote. Katika hekima Yake (Subhaanah) ni kuwa anamwongoza amtakaye na anampoteza amtakaye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (40) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatsah%20%20-%2028%20-%2012%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017