Kumuoa binadamu ambaye alinyonya kwa mama yangu

Swali: Dada yangu ni mdogo kwangu kwa miaka nane. Msichana wa ami yangu ana miaka hiyohiyo kama dada yangu na walinyonya ziwa moja. Mimi nataka kumuoa msichana wa ami yangu na mvulana wa ami yangu anataka kumuoa dada yangu. Kila mmoja anatoa mahari kivyake na si kupeana tu. Je, ndoa hii inafaa?

Jibu: Ikiwa dada yako alinyonya kutoka kwa mke wa ami yako basi si halali kwa mvulana wa ami yako. Kwa sababu atakuwa ni dada yake. Kadhalika ikiwa msichana wa ami yako alinyonya kutoka kwa mama yako basi si halali kwako. Kwa sababu atakuwa ni dada yako. Lakini tambua kwamba unyonyaji wenye kuharamisha ni ule wa kuvuta mara tano kabla ya kubaleghe. Kunyonya kwa kuvuta titi chini ya mara tano au kunyonya baada ya kubaleghe hakuna athari yoyote.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (11) http://binothaimeen.net/content/6755
  • Imechapishwa: 08/12/2020