Kumuitikia muadhini wakati wa darsa


Swali: Sisi tuko katika ukumbi tunasikiliza muhadhara chuoni. Tunasikia adhaana. Je, tumuitikia muadhini au tuendelee kusikiliza darsa? Hayo yanatutokea kila siku.

Jibu: Sunnah kwa yule yuko katika kazi yoyote pindi anapomsikia muadhini basi anatakiwa kumuitikia. Hata akiwa anasoma basi anatakiwa kusimamisha kisomo na kumuitikia muadhini. Wakiwa klasini basi yeye na wanafunzi wanatakiwa kusimamisha somo hili na waitikie. Hii ndio Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 20/10/2018