Kumuhijia mwengine hajj iliyopendekezwa

Swali: Je, inajuzu kumuhijia mtu ambaye ni muweza ikiwa ni hajj iliyopendekezwa?

Jibu: Kumuhijia mwengine hakukuthibiti isipokuwa kwa ambaye si muweza ikiwa hajj au ´umrah ni ya faradhi. Haya ndio yamepokelewa dalili. Hakukupokelewa dalili yoyote juu ya hajj au ´umrah iliyopendekezwa kwa ambaye yuhai. Ama kuhusu maiti inafaa kumuhijia, ni mamoja kitendo hicho ni cha wajibu au kimependekezwa. Lakini kuhusu aliyehai, haikuthibiti kumuweka mtu naibu isipokuwa kwa ambaye si muweza na hajj au ´umrah hiyo iwe ya wajibu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (22) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdatul-26-3-1435.mp3
  • Imechapishwa: 15/03/2020