Kumtumia maiti thawabu za swalah ya sunnah


Swali: Inajuzu kwangu kumswalia maiti swalah ya naafilah kisha kujaalia thawabu zake kumwendea yeye?

Jibu: Hakuna yeyote anayemswalia mwengine. Hakuna yeyote anayemswalia mwengine sawa awe hai au ameshakufa. Swalah ya ni kitendo cha kimwili na wala haichukui nafasi ya mwengine. Kama anataka kumnufaisha maiti amuombee du´aa, amtolee swadaqah, amuhijie au amfanyie ´Umrah. Kuna matendo yanayomwendea maiti ikiwa Allaah atayakubali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 22/10/2017