Swali: Mwanaume wa Kiislamu akimtukana mke wake au Dini yake anakuwa ni mwenye kutalikika Kishari´ah kama tunavyosikia kwa watu wengi?

Jibu: Akimtukana mke wake hatalikiki. Lakini ni juu yake atubu kwa Allaah na apatane na mke wake. Na ikiwa watasameheana, hakuna kitu. Na ikiwa atamtusi kama (mke) alivyomtusi kwa kulipiza kisasi bila ya kuzidisha juu ya hilo, haina neno. Na ikiwa atamsamehe ndio bora zaidi. Kwa kuwa Allaah Anasema:

اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ

“Fanyeni uadilifu; hivyo ni karibu zaidi na taqwa.” (05:08)

Ama kumtukania Dini yake ilihali naye (mwanamke huyo) ni Muislamu, huu ni ukafiri. Tunamuomba Allaah afya. Ikiwa mume ni Muislamu na mke ni Muislamu, kutukana Dini yake ina maana kautukana Uislamu. (Mke) asiishi naye (huyo mume). Atiwe adabu (huyo mume) na apigwe kwa kitendo chake hichi kibaya na aambiwe kutubia.Akitubu kwa kitendo chake hichi kibaya (ni vizuri) la sivyo ni wajibu (mume huyo) kuuawa. Ni wajibu kwa mtawala wa Waislamu au kiongozi wa nchi wamfanye atubu, la sivyo auawe. Kwa kuwa kutukana Dini ya Kiislamu ni katika aina mbaya kabisa za ukafiri zinazovunja Uislamu (wa mtu). Hali kadhalika kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutukana Qur-aan.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 25/03/2018