Swali: Kumuhijia maiti na kumtolea swadaqah zile gharama za hajj [mtu mwingine akahiji]. Ni lipi bora?

Jibu: Ikiwa maiti huyo bado hajahiji ile hajj ya kwanza ambayo ndio faradhi, basi hapana shaka kwamba lililo bora ni kumuwakilishia mtu wa kumfanyia hajj. Ama ikiwa ni hajj iliyopendekezwa mbali na ile ya kwanza, hapa atatakiwa kutazama manufaa: watu wakiwa ni wenye haja kubwa na wana uzito, basi kumtolea swadaqah ndio bora. Vinginevyo kumuhijia ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (53) http://binothaimeen.net/content/1198
  • Imechapishwa: 15/08/2019