Kumtolea salamu mtu ambaye nina mashaka ya Uislamu wake


Swali: Ni ipi hukumu ya kumtolea salamu mtu ambaye nina mashaka juu ya Uislamu wake? Ni ipi hukumu ya kuwatolea salamu watoto wa makafiri na kuwabusu? Ni ipi hukumu ya kumtolea salamu mwendawazimu na watoto wa waislamu?

Jibu: Mtu akiwa katika mji wa waislamu amtolee salamu yule anayekutana naye. Isipokuwa tu akijua kuwa sio muislamu yeye asianze kumtolea salamu. Yeye akianza kumtolea salamu basi amjibu kwa kusema:

وعليك

“Juu yako pia.”

kama ilivyokuja katika Hadiyth.

Kuhusu kuwatolea salamu watoto wa makafiri na kuwabusu sijui chochote kuhusiana na hili.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 28/04/2018