Kumtolea chakula mzee ambaye amekwishatokwa na akili

Swali: Ni ipi hukumu ya kumtolea chakula mtumzima mzee ambaye hajihisi mwenyewe?

Jibu: Mtumzima mzee ambaye hajihisi mwenyewe halazimiki si kulisha wala kufunga. Kwa sababu huyu ni kama mtoto mdogo ambaye hajakuwa na uwezo wa kupambanua au ambaye hajabaleghe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1565
  • Imechapishwa: 02/03/2020