Swali: Muislamu mwenye kueshi katika mji wa makafiri. Je, ni wajibu kwake kumtii raisi wa mji? Vipi tutajumuisha baina ya kumtii kafiri huyu na kukufuru Twaaghuut?

Jibu: Amtii katika yasiyokuwa maasi kwa Allaah. Asimtii katika ukafiri wala maasi. Ama katika mambo yanayoruhusu, hakuna neno. Lakini haijuzu kwake kueshi katika mji wa kikafiri ilihali ana uwezo wa kuhama kwenda katika miji ya waislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mhdr-09-11-1432.mp3
  • Imechapishwa: 20/09/2020