Swali: Kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz kwenda kwa ndugu muheshimiwa X (Allaah amuwafikishe). Salaamun ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh.

Nimefikiwa na barua yako ambayo ndani yake unaomba majibu juu ya maswali mawili ambapo moja wapo unauliza ni ipi hukumu ya kumtii baba yako katika kunyoa ndevu?

Jibu: Haijuzu kwako kumtii baba yako katika kunyoa ndevu. Bali ni lazima kuziacha na kuzifuga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yapunguzeni masharubu na fugeni ndevu, jitofautisheni na washirikina.”

“Hakika si venginevyo kutii kunakuwa katika yaliyo mema.”

Kufuga ndevu ni lazima na sio Sunnah kulingana na ile istilahi ya ki-Fiqh. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha hilo. Msingi wa maamrisho ni uwajibu na hakuna kitu kinachoyaondosha kutoka katika hali hiyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/93)
  • Imechapishwa: 09/08/2021