Swali: Baadhi ya Mashaykh wanayatibu maradhi kwa Aayah za Qur-aan. Ni upi usahihi wa kitendo hicho?

Jibu: Hapana shaka kwamba Allaah (Ta´ala) ameifanya Qur-aan hii kuwa ni ponyo kwa yale yaliyomo kifuani na ponyo juu ya yale yaliyomo kwenye mwili:

وَنُنَزِّلُ مِنَ الْقُرْآنِ مَا هُوَ شِفَاءٌ وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ

“Tunateremsha katika Qur-aan ambayo ni shifaa na rehema kwa waumini.” (17:82)

يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاءٌ لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ

“Enyi watu! Hakika yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu na shifaa ya yale yote yaliyomo vifuani, na mwongozo na Rahmah kwa waumini.” (10:57)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa, kama ilivyo katika Hadiyth ya Abu Sa´iyd ya kwamba walimsomea Ladiygh Suurah “al-Faatihah” mara saba. Akasimama akiwa na uchangamfu kama aliyetoka kwenye kifungo kikuu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema kuwaambia wale waliokuja kumweleza:

“Ni kipi kilichokujuza kwamba ni Ruqyah?”

Hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akathibitisha kuwa al-Faatihah ni Ruqyah anayosomewa mgonjwa. Qur-aan yote ni kheri na baraka. Hapana shaka kwamba inaathiri. Lakini ili Qur-aan iweze kuwa na taathira basi ni lazima yapatikane mambo matatu:

1- Msomaji awe na imani kuwa inaathiri.

2- Msomewaji awe na imani kuwa inaathiri.

3- Atayoyasoma dalili ziyasapoti kuwa yanaathiri.

Mambo yakiwa hivo basi itaathiri kwa idhini ya Allaah. Ama kukipungua moja wapo katika mambo haya matatu, kwa mfano mtu akasoma kwa njia ya kujaribu na kutaka kuona kama inasaidia au haisaidii, haitomfaa kitu. Kwa sababu ni lazima kwa muumini aamini kuwa inaathiri.

Kadhalika mgonjwa akiwa na mashaka juu ya hilo na hana imani juu ya kuathiri kwa Qur-aan haitomfaa kitu pia.

Vivyo hivyo akisoma Aayah ambazo dalili hazikuonyesha kuwa zinaathiri, kitendo hichi huenda pia kisilete taathira. Hiyo haina maana kwamba kuna upungufu katika Qur-aan tukufu. Hilo ni kosa katika usomaji wa yale ambayo hayatakiwi kusomwa katika Aayah au Suurah mbalimbali.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (10) http://binothaimeen.net/content/6739
  • Imechapishwa: 23/11/2020