Kumtaliki mke kwa ajili ya kutibu uchawi


Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa katika dawa ya kuondosha “Swarf” (uchawi wa mapenzi baina ya mume na mke), ni mume kumtaliki mke wake Talaka moja kisha uchawi utaondoka kwa idhini ya Allaah kisha atamrejea baada ya hapo. Je, maneno haya ni sahihi na unanasihi nini?

Jibu: Hii ni Fatwa ya ´Awwaam. Hakuna mwanachuoni yeyote aliyesema hivi. Wala sio sahihi. Kutibu uchawi si kwa Talaka, kutibu uchawi ni kwa kutumia dawa za Kishari´ah na si kwa kutoa Talaka. Na Allaah (Jalla wa ´Alaa) Anachukia Talaka isipokuwa kama kutakuwa haja (dharurah) ya kufanya hivyo kwa kukosekana maslahi au mapatano baina ya mume na mke. Ama kumtaliki kwa ajili ya dawa, sijui mwanachuoni yeyote aliyesema hivi. Hili limeenea kwa ´Awwaam.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/2927
  • Imechapishwa: 01/03/2018