Swali: Ipi hukumu kwa mwanamke kuonesha uso wake? Mwanamke ambaye hasikii maneno ya mume wake na anafunua uso wake, je inajuzu kumtaliki?

Jibu: Ndio. Kufuniko uso ni wajibu. Ni wajibu kwa mwanamke kufuniko uso wake kwa kuwandio ´Awrah kubwa kwenye mwili wake. Maono hutazama usoni mwa wanawake. Na wala hajulikani mwanamke mzuri kutokana na mbaya isipokuwa ni kwa (kutazama) uso wake. Uso ni fitina kubwa. Ni wajibu kwa dada wa Kiislamu kufunika uso wake kutokana na wanaume ambao sio Mahaarim zake. Na wala asijali ushawishi wa washawishi leo hii ambao wanatatiza suala la mwanamke kufuniko uso wake. Hakika Dini yake ndio imemlazimisha hilo. Na kumcha Allaah na kumtii Allaah na Mtume Wake ndio ambao wamemlazimisha.

Asijali upuuzi ambao unaenezwa hivi leo. Kufuniko uso kuna tofauti, kuna kadhaa na kadhaa. Wanachotaka ni mwanamke kuonesha uzuri wake au akae na wanaume naye ni mwenye kuonesha uzuri wa uso wake, wanja wake na vipodozi vya usoni mwake na kukaa nao kama jinsi anavyokaa na Mahaarim zake au mume wake. Haya zimepotea. Na hii ni njia ya kupotea kwa heshima yake na kuchukulia sahali heshima na karama ya mwanamke.

Mwanamke akiasi na akakataa kushikamana na Hijaab, mume wake amtaliki. Kwa kuwa haya ni maasi. Na wala haijuzu kwake kubaki nae hali ya kuwa anaendelea na maasi haya. Isitoshe jambo lingine ni kuwa, atawalea wasichana wake katika kufunua Hijaab. Kwa kuwa wasichana humuiga mama yao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=yJZUsvAkkY8
  • Imechapishwa: 07/02/2018