Kumtakia rehema muislamu mtenda madhambi makubwa

Swali: Je, inajuzu kumtakia rehema muislamu mtenda madhambi makubwa ambaye amekufa?

Jibu: Ndio, inajuzu kumtakia rehema na kumwombea du´aa ya msamaha. Ni kama ambavo anaswaliwa swalah ya jeneza akiwa ni mtenda madhambi na si kafiri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/395)
  • Imechapishwa: 11/03/2021