Swali: Je, mtu amtakie radhi Abu Sufyaan (Radhiya Allaahu ´anhu) wakati yanapotajwa matendo yake yaliyowadhuru waislamu?

Jibu: Ndugu! Kulipitika kwa makafiri yaliyo mabaya zaidi kuliko matendo ya Abu Sufyaan na wakati waliposilimu wakawa wanatakiwa radhi. Kulipitika kwa ´Umar kabla ya kusilimu kwake na kadhalika. Uislamu unafuta yaliyo kabla yake.

قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَنتَهُوا يُغْفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ

“Sema [uwaambie wale] waliokufuru: “Wakikoma basi watasamehewa yaliyopita.” (08:38)

Vipi unamtia aibu kwa kitu ambacho Allaah Amemsamehe kwacho? Haijuzu kufanya hivi kwa Abu Sufyaan wala mwengine asiyekuwa yeye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (58) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13521
  • Imechapishwa: 16/11/2014