Kumtaja Allaah kwa moyo daima na kila maeneo

Swali: Ni jambo linalotakikana kwa mtu kumtaja Allaah katika kila wakati na katika kila hali isipokuwa katika yale maeneo ambayo kuna makatazo ya kumtaja Allaah ndani yake kama mfano bafuni. Je, mtu asitishe kabisa kumtaja Allaah bafuni ijapo ni ndani ya moyo wake?

Jibu: Kumtaja Allaah ndani ya moyo ni jambo limewekwa katika Shari´ah katika kila wakati na maeneo. Ni mamoja bafuni na kwenginepo. Kilichochukizwa bafuni ni kumtaja Allaah kwa mdomo hali ya kumtukuza Allaah (Subhaanah). Isipokuwa tu kumtaja Allaah wakati wa kutawadha. Mtu anatakiwa kumtaja Allaah asipopata wepesi wa kumtaja Allaah nje ya bafu. Kwa sababu baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa ni lazima na kikosi cha wanazuoni wengi wanaona kuwa ni Sunnah iliyokokotezwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/32)
  • Imechapishwa: 30/07/2021