Kumswalia Mtume kwa dhamiri


Swali: Baadhi ya watu wanapotaka kumnasibishia Mtume (Swalla Allaahu  ´alayhi wa sallam) basi husema:

“Amesema (Swalla Allaahu  ´alayhi wa sallam).”

Hawasemi “Mtume (Swalla Allaahu  ´alayhi wa sallam) amesema” au Muhammad (Swalla Allaahu  ´alayhi wa sallam) amesema. Katika hali kama hii mtu aitikie “Aamiyn” au na yeye amswalie?

Jibu: Hapana shaka kwamba hapa dhimiri ya “amesema” inarejea kwa Mtume (Swalla Allaahu  ´alayhi wa sallam). Udhahiri ni kwamba dhamiri ni kama mtu ametaja. Ndani yake kunaingia maneno ya Mtume (Swalla Allaahu  ´alayhi wa sallam) kutoka kwa Jibriyl aliyesema:

“Ameangukia pua yule ambaye nitatajwa mbele yake asiniswalie.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (15) http://binothaimeen.net/content/6800
  • Imechapishwa: 17/02/2021