Kumswalia Mtume baada ya adhaana – Sunnah au Bid´ah?

Swali: Baada ya kila adhaana muadhini husema:

الصلاة والسلام عليك يا سيدي يا رسول الله، يا من في المدينة المنورة صلاة وسلاماً دائماً عليك

“Swalah na salamu ziko juu yako, ee bwana wangu, ee Mtume wa Allaah, ee uliyoko katika mji Mtukufu – salamu na swalah daima ziwe juu yako.”

Je, haya ni katika Bid´ah?

Jibu: Ndio. Naapa kwa Allaah kwamba haya ni katika Bid´ah. Ni lazima kuyasitisha. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisisitiza kumswalia na kumtakia amani kisha kumuombea du´aa ya wasiylah. Pindi muadhini anapomaliza kutoa adhaana atasema:

اللهم صلي على محمد، اللهم رب هذه الدعوة التامة والصلاة القائمة، آت محمداً الوسيلة والفضيلة، وابعثه مقاماً محموداً الذي وعدته إنك لا تخلف الميعاد

“Ee Allaah, Mola wa mwito huu uliotimia, swalah iliosimama, mpe bwana wetu Muhammad, Wasiylah na fadhilah na mfikishe daraja yenye kusifiwa ambayo umemuuahidi. Kwani hakika wewe huendi kinyume na miadi.”

Vivyo hivyo ndivo atasema yule ambaye alikuwa akimuitikia muadhini. Lakini [muadhini] asiyaseme haya kwenye kipaza sauti au juu ya minara. Ayasema haya ndani ya nafsi yake. Kwa sababu matamshi ya adhaana yamehifadhiwa na kunukuliwa kwa njia nyingi kati ya waislamu. Ndani yake hakuna nyongeza hii. Du´aa inaombwa kimyakimya na sio kwa sauti ya juu.

Muulizaji: Je, muadhini anapata dhambi iwapo ataendelea kufanya hivo?

Ibn ´Uthaymiyn: Ndio, anapata dhambi. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitahadharisha kutokamana na Bid´ah matahadharisho makali. Amesema:

“Kila Bid´ah ni upotevu.”

Hivi kweli mtu anaweza kuthubutu juu ya upotevu kwa kila wakati? Khasa ukizingatia kwamba anaita katika swalah na kufaulu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (377) http://binothaimeen.net/content/13367
  • Imechapishwa: 24/10/2020