Swali: Ikiwa maiti ameacha deni haswaliwi mpaka alipe lile deni, ni jambo limewekwa katika Shari´ah yanayofanywa na baadhi ya watu anasimama mbele ya maiti kabla ya kuswali na kusema “Aliye na deni kwa maiti huyu basi mimi nitalibeba”?

Jibu: Hili ni jambo zuri. Lakini kujibebesha nalo haitoshi, bali ni lazima kulilipa. Kama mnavyojua maiti akiwa na deni hata kama halikubeba yeyote anaswaliwa na watu, lakini Mtume yeye peke yake ndiye hatakiwi kumswalia. Ama wengine wanatakiwa kumswalia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-10-29.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014