Kumsusa shangazi ambaye amewaoza Raafidhwah


Swali: Je, inajuzu kumkata shangazi yangu na kutoungana naye kwa sababu amemuozesha msichana wake kwa Raafidhwiy anayewatukana Maswahabah?

Jibu: Ikiwa amekusudia hili na wewe unajua hili na ulimshauri lakini hata hivyo hakukubali, hakuna shaka yoyote ya kwamba ni wajibu kwako kumkata na kujitenga naye mpaka atapotubu kwa Allaah (´Azza wa Jall). Huku ni kususa kwa haki. Kumsusa mwenye kufanya maasi ikiwa hakutekeleza na hakukubali ni jambo limewekwa katika Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus al-Masjid al-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13980
  • Imechapishwa: 04/04/2018