Kumsomea maiti Qur-aan, kumchinjia na kumfanyia walima


Swali: Huku kwetu watu wanawasomea Qur-aan maiti na wanachukua ujira kwa hilo. Anapokufa mmoja wao wanamsomea Qur-aan kwa siku tatu, wanamchinjia na kumfanyia walima. Je, maiti wanafaidika kwa lolote na je hili ni katika Shari´ah?

Jibu: Hili ni Bid´ah. Kumsomea maiti na kuchukua ujira kwa hilo, hili ni Bid´ah na wala halijuzu. Hakuna cha ujria na wala haifai kwake kumsomea maiti na wala hakuna dalili ioneshayo kuwa atanufaika kwayo, bali hili ni munkari na Bid´ah. Hali kadhalika, kumchinjia na kumfanyia chakula, yote haya ni Bid´ah na munkari na hayajuzu. Ni wajibu kutahadhari hilo na kuwatahadharisha watu kwa hilo. Hili ndilo la wajibu kwa wanachuoni na kwa watawala. Wawatanabahishe watu kwa Aliyokataza Allaah, na wawachukulie hatua wajinga na wapumbavu mpaka waweze kunyooka katika njia iliyonyooka ambayo Allaah Kawawekea nayo waja Wake. Kwa hilo, hali na jamii itatengemaa, na itadhihiri hukumu ya Kiislamu na mambo ya Kijaahiliyyah yataisha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 25/03/2018