Kumsapoti dhalimu


Swali: Ni vipi tutaonisha kati ya maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”[1]

na Hadiyth isemayo:

“Yule mwenye kutembea na mtu dhalimu kwa ajili ya kumpa nguvu ilihali anajua kuwa ni dhalimu, basi kwa hakika ametoka nje ya Uislamu.”[2]?

Jibu: Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”

Tumekwishazungumza kuhusu Aayah hii. Tumesema kuwa tusiwe na matumaini makubwa ambapo tukafanya maasi ambayo ni chini ya shirki kwa kutumai kwamba yanaingia ndani ya matakwa. Kwani wewe una uhakika kwamba Allaah anataka kukusamehe? Hapana. Hivyo basi usighurike na matumaini yanayotokana na Aayah hii.

Ama kuhusu Hadiyth uliyoashiria, mimi siijui. Lakini endapo itakuwa ni Swahiyh, basi inahusiana na yule ambaye atatembea na dhalimu ambaye amefanya dhuluma inayomtoa nje ya Uislamu ambapo akamnusuru. Basi katika hali hiyo na yeye pia anakuwa ni mwenye kutoka nje ya Uislamu.

[1] 04:48 na 116

[2] al-Bayhaqiy katika ”Shu´b-ul-Iymaan” (6/2606). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf-ul-Jaamiy´” (5859).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=dyPFvV7Ngnw&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 06/09/2020