Swali: Je, lini bora kwa ambaye yuko karibu na msomaji Qur-aan; je, amsalimie na ampe mkono baada ya kumaliza kwake kuswali swalah ya mamkuzi ya msikiti au bora ni kutomkata kisomo chake na kumshughulisha na kisomo?

Jibu: Sunnah ni yeye kusalimiwa na kupewa mkono. Hayo ni kutokana na yale yaliyothibiti katika Hadiyth ambazo ni Swahiyh kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Watapokutana waislamu ambapo wakapeana mikono, basi yanapukuchika madhambi yao kama yanavopukuchika kutoka kwenye mti wenye majani makavu.”

Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakikutana basi wanapeana mikono na wanapofika kutoka safarini wanakumbatiana.”[1]

Amepokea ad-Daaraqutwniy. Wapokezi wake ni wenye kujengewa hoja katika “as-Swahiyh”.

Jengine ni kwa sababu katika kufanya hivo kuna kuyasisitiza yale mapenzi, kuliwazana na kufahamiana kati ya waislamu. Kukata kisomo kutokana na manufaa yaliyozuka ni jambo linalotakikana.

[1] Haythamiy (08/36) na akasema:

”Ameipokea ad-Daaraqutwniy katika ”al-Awsatw na wapokezi wake ni wapokezi wa Swahiyh, ameipokea pia al-Bayhaqiy (07/100) na katika ”Silsilah Ahaadiyth as-Swahiyhah” (160) ya al-Albaaniy.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/433)
  • Imechapishwa: 19/11/2021