Kumposa mwanamke mtalikiwa wakati wa eda yake

Swali: Inajuzu kumchumbia mwanamke mtalikiwa ndani ya eda yake?

Jibu: Hapana, haijuzu kumposa mwanamke ambaye ana talaka rejea ndani ya eda yake. Ni mke wa watu mpaka eda yake itapokwisha. Usimchumbie maadamu bado yuko chini ya mume wake.

Kuhusiana na mwanamke ambaye mume wake hawezi kumrejea, mtu anaweza kumchumbia kwa kumuashiria na sio kumwambia moja kwa moja ndani ya eda yake:

وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُم بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ أَوْ أَكْنَنتُمْ فِي أَنفُسِكُمْ

“Wala si dhambi juu yenu katika mliyotolea ishara kwayo ya kuposa wanawake [walio katika eda] au mliyoficha katika nafsi zenu.” (02:235)

Mwambie kuwa unataka kuoa, kwamba unatafuta mke na maneno mengine kwa ishara. Hata hivyo haifai kumwambia kwa njia ya moja kwa moja ya kwamba unataka kumuoa wakati atapomaliza eda:

وَلَـٰكِن لَّا تُوَاعِدُوهُنَّ سِرًّا إِلَّا أَن تَقُولُوا قَوْلًا مَّعْرُوفًا

“… lakini msifunge nao ahadi kisiri isipokuwa mseme kauli njema.” (02:235)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdh–14340126_0.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020