Kumpiga picha bwanaharusi au bibiharusi

Swali: Ni ipi hukumu ya kumpiga picha bwanaharusi katika ndoa kwa ajili awe na kumbukumbu na ili wamuone wale ndugu na marafiki ambao hawakuhudhuria ndoa? Pamoja na kuzingatia kwamba anayepigwa picha ni bwanaharusi tu na si bibiharusi.

Jibu: Naona kuwa hakuna haja ya kufanya hivo. Wanawake wote wanatamani kuolewa kama ambavo wanaume pia wote wanatamani kuoa. Lakini tatizo ima linatokana na mawalii wao au ni kutokana na ukubwa wa mahari na uzito wake. Inawezekana vilevile ikawa tatizo ni kuwa mwanamke anataka kubaki anaendelea na kazi yake ya masomo; ima mwalimu au mwanafunzi. Huenda pia zipo sababu zengine. Kule mwanamke kutotamani kuolewa isipokuwa mpaka akiona picha ya dada yake ni jambo lisilomsaidia kitu. Kwa ajili hiyo naona kuwa  picha hii ni haramu na haijuzu. Baya kuliko hayo ni mwanaume na mumewe wapigwe picha pale wanapokutana kwa mara ya kwanza na khaswakhaswa ikiwa ni kwa kuwachukua video camera. Kwa sababu video camera inasimulia picha ya aliyehai kabisa.

Kwa hiyo ni wajibu kwetu kumcha Allaah (´Azza wa Jall):

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ

“Na yeyote anayemcha Allaah, basi atamjaalia njia ya kutokea.” (65:02-03)

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مِنْ أَمْرِهِ يُسْرًا

“Na yeyote anayemcha Allaah, basi atamjaalia wepesi katika jambo lake.” (65:04)

Matamanio na kutaka kuwafurahisha watu kusitupelekee katika shari na uharibifu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (47) http://binothaimeen.net/content/1079
  • Imechapishwa: 03/07/2020