Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

13- Abu Hamzah Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) mtumishi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza kwamba Mtume amesema:

“Haamini mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake kile anachojipendelea juu ya nafsi yake.”

Hili linahusu matendo yote ambayo ni mema, katika maneno, matendo na I´tiqaad. Hili ni pamoja na mtu kumpendelea ndugu yake aamini imani sahihi kama anavyoamini yeye. Hili ni jambo la wajibu. Ampendelee ndugu yake naye awe ni mwenye kuswali kama anavyofanya yeye. Akimpendelea ndugu yake awe kinyume na uongofu, anakuwa amefanya tendo la haramu na hivyo anakuwa hana ukamilifu wa imani ilio ya wajibu. Lau atampendelea fulani miongoni mwa watu awe kinyume na I´tiqaad sahihi inayoafikiana na Sunnah, kwa msemo mwingine awe katika I´tiqaad za ki-Bid´ah, kadhalika atakuwa hana ukamilifu wa imani ilio ya wajibu. Hili linahusu pia mambo mengine yote ya ´ibaadah na aina mbali mbali ya kuepuka mambo ya haramu.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 220-221
  • Imechapishwa: 16/05/2020