Kumpeleleza anayehisiwa kuuza dawa za kulevya

Swali: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza jambo la kupelelezana. Je, inafaa kuwapeleleza mapromota au wauzaji [dawa za kulevya] ili kuwatega?

Jibu: Ndio. Huko sio kupeleleza. Kufanya hivo ni kutoa nasaha kwa ajili ya Allaah na kuwatakia mema waja. Akijulikana promota na msafirishaji basi ni sawa kumpeleleza mpaka zijulikane khabari zake na lipelekwe jambo lake kwa watawala. Huyu madhara yake ni yenye kuenea. Ni tofauti na yule anayetumia mwenyewe na mtenda madhambi ambaye dhambi inakuwa kati yake yeye na Allaah. Huyu ndiye mwenye kusitiriwa na kutopelelezwa. Kuhusu ambaye anawadhuru watu, anaeneza shari yake na anasambaza usifadi, huyu madhara yake ni makubwa na madhara yake ni yenye kuenea kwa wengine. Amefanana na majambazi bali ni mwenye madhara zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4419/حكم-التجسس-على-مروجي-المخدرات-ونحوها
  • Imechapishwa: 17/06/2022