Swali: Kuna mtu amesahau baadhi ya kanda za muziki kwangu na sijamrejeshea nayo mpaka hivi sasa. Je, nimrudishie?

Jibu: Hapana, maadamu ina muziki usimrudishie. Bali ivunje au uifute na badala yake uweke kitu chenye faida katika Qur-aan au mihadhara. Ama kumrudishia nayo ilihali ina muziki haijuzu kufanya hivi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (16) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-03-07.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014