Kumpata mtu kwa kijicho ni jambo kweli lipo?

Swali: Je, kuogopa kupatwa na kijicho kunapingana na kumtegemea Allaah?

Jibu: Hapana, hakupingani kwa sababu ni sababu ilio wazi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kijicho ni haki. Kama kuna kitu chenye kuitangulia Qadar basi kijicho kingeitangulia.”

Hii ni Hadiyth Swahiyh. Kijicho ni haki. Allaah amewaumba baadhi ya watu na macho ya namna hiyo. Baadhi ya watu macho yao yana sumu, hivyo ndivyo alivyosema Ibn-ul-Qayyim. Wanawasibu wengine kwa kijicho. Wanapowatazama wengine wanawaathiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (70) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighatsah%20-%2019%20-0%207%20-%201438.mp3
  • Imechapishwa: 10/09/2017