Kumpasua mwanamke ambaye kafariki na tumboni mwake kuna mtoto hai


Swali: Lau mwanamke anakufa na tumboni mwake ana kijusi (mtoto) ambaye yuko hai. Je, inajuzu kwa tabibu kupasua tumbo lake?

Jibu: Sioni kama kuna makatazo yoyote ya hili, hakuna ubaya In Shaa Allaah kupasua tumbo lake na kumtoa mtoto nje.

Muulizaji: Baadhi yao (madaktari) wanawaua.

al-Waadi´iy: Kuwaua haijuzu. Haijuzu kumuua mtoto.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=381
  • Imechapishwa: 02/03/2018