Swali: Wakati mwingine najiwa na mwendawazimu anayeniomba pesa na anataka kununua chakula. Je, nimpe pesa au naingia katika Kauli Yake (Ta´ala):

وَلَا تُؤْتُوا السُّفَهَاءَ أَمْوَالَكُمُ الَّتِي جَعَلَ اللَّـهُ لَكُمْ قِيَامًا

“Wala msiwape wendawazimu mali zenu ambazo Allaah Amekujaalieni kuwa ni msingi wa kujipatia riziki… “ (04:05)

Jibu: Mpe walii wake. Mwendawazimu lazima awe na walii. Mpe walii wake ili aweze kumhudumia na kumnunulia haja zake. Ukimpa mwendawazimu atazichana na hawezi kuzitumia vizuri. Ataziangamiza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (14) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-1-24.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014