Swali: Je, inafaa kwangu kupeana mkono na dadake mke wangu, kukaa naye chemba na mengineyo kwa sababu najua kuwa ni Mahram yangu?

Jibu: Haijuzu kwako kupeana mkono na dadake mke wako wala kukaa naye chemba. Sio katika Mahaarim zako. Ni wa kando nawe. Hali yake ni kama wanawake wengine wote katika jambo hilo. Jihadhari kuchukulia wepesi na kuzama katika jambo hilo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/حكم-مصافحة-أخت-الزوجة
  • Imechapishwa: 12/06/2022