Swali: Inajuzu kuwapa nyama ya Udhhiyah wasiokuwa waislamu?

Jibu: Hakuna neno kuwapa. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّـهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ

“Allaah hakukatazeni kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiokupigeni vita katika dini na wala hawakukutoeni kutoka majumbani mwenu. Hakika Allaah anapenda wenye kufanya uadilifu.” (60:08)

Makafiri ambao hakuna kati yetu sisi na wao vita. Bali kafiri ambaye kuna amani au mikataba ya amani baina yetu anaweza kupewa katika Udhhiyah na swadaqah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/14499/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D8%B9%D8%B7%D8%A7%D8%A1-%D8%A7%D9%84%D9%83%D8%A7%D9%81%D8%B1-%D9%85%D9%86-%D9%84%D8%AD%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%B6%D8%AD%D9%8A%D8%A9
  • Imechapishwa: 17/08/2018