Kumpa chakula mfanyakazi kafiri mchana wa Ramadhaan

Swali: Kuna mkulima ana wafanya kazi Misri lakini hawaswali na wala hawafungi. Wakati alipowaamrisha kuswali na kufunga hawakumkubalia na wakamuomba awape chakula mchana wa Ramadhaan. Vinginevyo wataacha kazi wakidai kwamba sio waislamu. Akawapa chakula katika Ramadhaan. Unasemaje juu ya jambo hilo?

Jibu: Mosi kuwatumia wafanya kazi ambao si waislamu ni jambo lisilotakikana na lisilostahiki. Inatakikiana kuacha kuwatumia wafanya kazi wasiokuwa waislamu. Kwa sababu kuwatumia wafanya kazi wasiokuwa waislamu ni kitu kinachoweza kumdhuru mtu mwenyewe, katika ´Aqiydah yake au tabia yake. Ni jambo pia linaweza kuwadhuru watoto na familia yake na khaswa wale wafanya kazi na walezi wa kike. Hawa wanawake hao madhara yao ni makubwa.

Kuhusu kuwapa chakula ni kitu kisichojuzu wakiwa sio waislamu na wakataka kupewa chakula katika Ramadhaan, asifanya hivo. Asiwasaidie juu ya jambo hilo hata kama msingi wao kweli ni makafiri na funga haisihi kwao. Lakini hata hivyo ni wenye kuzungumzishwa kwa matawi ya Shari´ah. Mambo yakishakuwa ni hivo basi haijuzu kuwasaidia kwa mambo yanayokwenda kinyume na Shari´ah. Bali anapaswa kuwanasihi na kuwaelekeza pengine wakaingia ndani ya Uislamu. Wanatakiwa kulinganiwa katika Uislamu na kuelekezwa katika kheri pengine wakasilimu na hivyo mtu huyo akapata thawabu mfano wa yule aliyeelekeza katika kheri ambapo anapata thawabu mfano wa yule mtendaji. Ukiongozewa mtu mmoja peke yake ni bora kwako kuliko ngamia wekundu walionona. Hivi ndivo alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Wakikataa basi wajipikie chakula wenyewe. Wao wenyewe ndio wanatakiwa kujisimamia haja zao juu ya jambo hili. Pengine wakaathirika kwa jambo hilo na hivyo wakaingia katika Uislamu. Vinginevyo ivunjwe mikataba yao na Allaah ataleta wabora kuliko wao. Asiwachukulie wepesi hata kama watamtisha kuacha kazi. Wakiacha kazi waache na Allaah atamletea wabora kuliko wao. Haitakikani kabisa kuwasaidia juu ya kula na kunywa katika Ramadhaan. Ni mamoja watu hao ni makafiri au waislamu watenda madhambi ambao hawafungi. Haifai kwa mtu kusaidia juu ya yale aliyoharamisha Allaah. Haijalishi kitu mtu huyo ni kafiri au muislamu mtenda madhambi. Asiwasaidie. Wanaweza kujinunulia na kujipikia wenyewe kile wanachohitaji.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/4195/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%AA%D9%82%D8%AF%D9%8A%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B7%D8%B9%D8%A7%D9%85-%D9%84%D9%84%D8%B9%D9%85%D8%A7%D9%84-%D8%BA%D9%8A%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B3%D9%84%D9%85%D9%8A%D9%86-%D9%81%D9%8A-%D9%86%D9%87%D8%A7%D8%B1-%D8%B1%D9%85%D8%B6%D8%A7%D9%86
  • Imechapishwa: 01/05/2020