Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kuomnyonyesha mtoto wake baada ya miaka miwili? ´Allaamah Muqbil al-Waadi´iy: Sioni ubaya wowote wa hilo. Ama Kauli Yake (Ta´ala):

وَالْوَالِدَاتُ يُرْضِعْنَ أَوْلَادَهُنَّ حَوْلَيْنِ كَامِلَيْنِ

“Na wazazi wa kike wanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili.” (02:233)

Hii ndio aghlabu ya watoto wengi. Lakini lau mtoto atakataa, akamnyonyesha mwezi mmoja, miwili, mitatu au minne, sioni ubaya wowote wa hili.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=756
  • Imechapishwa: 02/03/2018