Kumnyoa nywele mtoto wa kike katika ´Aqiyqah


Swali: Mtu akipata mtoto wa kiume basi imesuniwa kunyoa kichwa cha mtoto huyo na kutoa swadaqah kwa kiasi cha zile nywele. Kuhusiana na mtoto wa kike imesuniwa juu yake kufanya hivo au mtu atoe swadaqah moja kwa moja?

Jibu: Hapana. Haijuzu kwa haki ya mtoto wa kike. Mtoto wa kike hanyolewi kichwa chake. Kunyolewa ni jambo linalowahusu watoto wa kiume tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahssat.mp3
  • Imechapishwa: 25/09/2018