Kumnasihi imamu anayeswali mwendokasi

Swali: Sisi tuna imamu msikitini anaswali haraka sana kiasi cha kwamba hatuwahi kusema Adhkaar za Rukuu´ na Sujuud. Tufanye nini?

Jibu: Ni lazima kwa imamu huyu na wengine kutulia ndani ya swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomuona yule bwana anayefanya haraka ndani ya swalah yake alimwambia:

“Rejea ukaswali. Kwani hakika hujaswali.” Kisha akasema: “Unaposimama kutaka kuswali, lete Takbiyr. Kisha soma uwezacho katika Qur-aan. Kisha utarukuu mpaka unyooke. Kisha utasimama sawasawa. Kisha utasujudu mpaka utapotulia katika Sujuud. Kisha utainuka na kutulia katika kikao kisha utafanya hivyo katika swalah zote.”[1]

Ni lazima kumnasihi imamu huyu na mumweleza kuwa kutulia ndani ya swalah ni moja katika nguzo za swalah. Mukhofisheni juu ya Allaah na mumweleza kuwa swalah yenu hiyo ni amana juu ya shingo yake na hivyo atulie ndani yake. Imekuja katika Sunan ya Abu Daawuud na at-Tirmidhiy na “al-Musnad” ya Imaam Ahmad ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Imamu ni mdhamini na muadhini ameaminiwa. Ee Allaah! Waongoze maimamu na wasamehe waadhini.”[2]

[1] al-Bukhaariy (757), Muslim (397), at-Tirmidhiy (303) na wengineo.

[2] at-Tirmidhiy (207), Abu Daawuud (517) na Ahmad (02/461).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/الواجب-على-الامام-الاطمئنان-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 18/06/2022