Swali: Ikiwa mtu ameingia katika Uislamu karibuni mtu aende naye daraja baada ya nyingine kwa kumbainishia mambo ya faradhi? Kwa mfano lau atasilimu kabla ya Ramadhaan kwa siku mbili, je, tumlazimishe swawm au tumuache mpaka Uislamu wake uwe na nguvu?

Jibu: Hakusilimu isipokuwa ni kwa sababu anataka Uislamu na anataka kuokoka na Moto. Kwenda kwa daraja ni kwa Allaah na si kwetu sisi. Yeye ndiye anayefanya kwenda hatua kwa hatua na kuweka Shari´ah. Tunatakiwa kumweleza kuhusu swawm na kumuamrisha nayo. Akikataa basi anaritadi. Akisilimu na akakataa kufunga, baada ya kubaleghe na kuijua, anaritadi katika dini ya Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (15) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-02-09.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014